Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imekutana na wadau wa Fasihi Andishi (Kiswahili na Kiingereza) kwa lengo la kupitia miongozo ya kuchagua vitabu vya fasihi kwa ajili ya kutumika katika shule za sekondari na vyuo vya Ualimu nchini.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano TET na kimeongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt.Aneth Komba.
Miongozo hiyo ambayo imeandikwa kutokana na umuhimu wa kuwa na vitabu vya fasihi andishi vinavyokidhi mahitaji ya sasa imeandaliwa na wataalamu bobezi kutoka TET na vyuo vikuu.
Baada ya kupitia na kuweka maboresho, miongozo hiyo itaendelea na hatua muhimu za uithinishaji ili kuweza kutumika shuleni na vyuoni.