Wafanyabiashara wa Tanzania na Italia kukutanishwa

0
148

Ubalozi wa Italia nchini kwa kushirikiana na Wakala wa Biashara wa nchi hiyo (ITA), umeandaa jukwaa la pili la biashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Italia.

Jukwaa hilo litafanyika kuanzia Septemba 27 hadi 30 mwaka huu, katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Mada mbalimbali zitawasilishwa wakati wa jukwaa hilo la pili la biashara kati ya Tanzania na Italia ambazo ni pamoja na kilimo biashara, utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundombinu na uchumi wa buluu.