Ukata wakwamisha timu ya taifa ya Kikapu

0
253

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) limeeleza kuitoa timu taifa ya wavulana ya mpira wa kikapu kushiriki mashindano ya Afrika ya kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 18.

Taarifa ya TBF inasema, timu hiyo sasa haitashiriki kwenye mashindano hayo ya siku 10 yatakayofunguliwa Agosti 4 nchini Madagascar kutokana na ukata.

“Shirikisho limekosa pesa za kuipeleka timu ya wavulana, hivyo msimu huu tutawakilishwa na timu ya wasichana pekee,” imeeleza taarifa ya TBF.

Taarifa hiyo imesema Tanzania ilipata uwakilishi wa timu mbili ya wavulana na wasichana kwenye mashindano hayo yanafanyika kulingana na kalenda ya Shirikisho la kikapu Afrika (FIBA Afrika).