Rais ateua wakuu wa mikoa wapya 9

0
195

Rais  Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya tisa , kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa mikoa saba  na wengine 10 kubakia kwenye vituo vyao.

Wakuu wa mikoa wapya ni 

Nurdin  Babu  ambaye  ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kabla ya uteuzi huo  alikuwa mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Fatma  Mwasa ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro,  Halima Dendego ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa na Raphael  Chegeni  ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara.

Wengine ni Peter  Serukamba aliyeteuliwa  kuwa mkuu wa mkoa wa Singida, Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara ambapo kablla ya uteuzi huo alikuwa mkuu wa qilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

Kanali Laban Thomas ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma na  alikuwa Mkuu wa wilaya ya Nyasa kabla ya uteuzi huo, Albert  Chalamila yeye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera.

Dkt. Yahaya Nawanda  ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu na kabla ya uteuzi huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Tabora mkoani Tabora.