Yanga kulamba bilioni 12 kutoka Sportpesa

0
193

Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa, imesaini mkataba wa kuendelea kuidhamani klabu ya soka ya Yanga wenye thamani ya shilingi bilioni 12 kwa kipindi cha miaka mitatu.

Yanga Sc imesaini mkataba huo mara baada ya mkataba wa awali kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Yanga imewakilishwa na Rais wake Mhandisi Hersi Said huku Sportpesa ikiwakilishwa na Mkurugenzi wa uendeshaji wa kampuni hiyo Abbas Tarimba.