LATRA : Marufuku biashara na mahubiri ndani ya basi

0
159

Wafanyabiashara na wahubiri wanaofanya shughuli zao ndani ya mabasi wamepigwa marufuku kuendelea na shughuli hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) Habibu Suluo amesema, kufanya biashara na mahubiri ndani ya basi ni kinyume cha kanuni za mamlaka hiyo.

“Biashara kwenye mabasi marufuku, wale wenye kutoa mahubiri kwenye mabasi marufuku, ni kanuni. Tukikuta mwenye basi anaruhusu hivi tutakuwa na namba zetu tukipata taarifa tukitoa adhabu itakuwa sio jambo zuri, tuzingatie kanuni usiumize hisia za mtu.” amesema Suluo