Ujenzi wa Tangi Kilindini kuwapa unafuu wa maji Kaskazini Pemba

0
240

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi amesema ujenzi wa mradi tangi la kuhifadhia maji eneo la Kilindini litasaidia kuwatua ndoo kichwani akina mama wa jimbo la Wingwi kwa kupata maji ya uhakika.

Rais Dkt. Hussein Mwinyi Amesema hayo leo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tangi la kuhifadhi maji eneo la Kilindini lililopo Wilaya ya Micheweni katika muendelezo wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoa wa Kaskazini Pemba.