Serikali yatoa siku 67 MSD ifumuliwe

0
276

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai, kuhakikisha anapangua safu ya uongozi pamoja na wafanyakazi wengine wa chini wa taasisi hiyo.

Waziri Ummy Mwalimu ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa bodi ya MSD itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Rosemary Slaa.

Mara baada ya kuizindua bodi hiyo, ameipa jukumu la kuhakikisha inasimamia suala hilo la kupangua safu ya uongozi pamoja na wafanyakazi wa MSD.

Ametoa muda wa siku 67 kuanzia leo hadi Septemba 30 mwaka huu kukamilisha kazi ya kuifumua Bohari ya Dawa kiutendaji.

Waziri Ummy Mwalimu ameitahadhari Bohari ya Dawa kwa kusema kuwa biashara ya dawa ni miongoni mwa biashara hatari, hivyo wanapaswa kuwa makini wakati wa utendaji wao.

Amesema awali MSD ilifanya kazi vizuri na kuaminiwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), hivyo ameagiza kurudishwa kwa mifumo ya TEHAMA iliyosaidia kudhibiti mianya ya ubadhirifu ndani ya taasisi hiyo.