Vijana watakiwa kuthamini Vipaji vyao

0
155

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi amewaasa vijana nchini kutambua na kuthamini vipaji vyao ili waweze kufikia malengo waliojiwekea na kuleta tija kwenye jamii inayowazunguka.

Akizunguza Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Mzalendo Project Foundation iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Naibu Waziri huyo emesema azma ya serikali ni kuendelea kuwajengea vijana mazingira rafiki yatakayowawezesha kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

“Serikali ipo tayari wakati wote kutoa msaada wa hali na mali kuhakikisha vijana wanapata fursa za ajira na upatikanaji wa mitaji itakayo wawezesha kujishughulisha na kazi ambazo zitakazowaingizia kipato,” Amesema Katambi

Pia Niabu Waziri Katambi ameeleza mikakati ya Serikali katika kutumia tafiti zilizofanyika na wataalam mbalimbali kwa lengo la kuangalia namna nzuri ya kupunguza changamoto ya ajira Kwa wananchi wake hususani kundi la vijana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Project Foundation (MZPF) Enock Mwesiga amesena lengo la taasisi hiyo ni kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wa Vyuo vikuu nchini mara baada ya kumaliza elimu yao ya juu, .

Msanii wa Kizazi Kipya Kala Jeremiah, ameeleza kuguswa na vijana hao ambao wameonyesha uthubutu kwa kuanzisha taasisi hiyo nakutoa Wito Kwa vijana kuthamini muda ili waweze kufikia ndoto zao na malengo waliyojiwekea.