Tanzania yaichapa Somalia 1-0

0
249

Tanzania imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN) mwakani nchini Algeria.

Goli la Tanzania limefungwa katika dakika ya 46 na Abdul Suleiman ‘Sopu’ na hivyo kuiweka Tanzania kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye hatua ya pili ya michuano hiyo.

Mchezo wa marudiano baina ya mataifa hayo utapigwa Julai 30 mwaka huu ambapo mshindi wa jumla atasonga mbele kwenye mechi za mchujo zitakazofikia tamati Septemba 2, mwaka huu.

Fainali za CHAN zilikuwa zifanyike Julai 10 hadi Agosti 1, mwaka huu lakini Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likasogeza hadi mwakani kutokana na kuahirishwa kwa fainali zilizopita sababu kubwa ikiwa ni janga la UVIKO19.