SABA TV mbioni kuanzishwa

0
162

Wakurugenzi wakuu na watendaji wa mashirika ya Utangazaji Kusini mwa Afrika (SABA), wanajadili juu ya uanzishwaji wa chaneli mpya ya televisheni ya SABA TV kwenye kikao cha bodi ya SABA kinachoendelea nchini Namibia.

Miongoni mwa wakurugenzi wakuu wanaoshiriki kikao hicho ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha.

Lengo kuu la chaneli hiyo ambayo uzinduzi wake wa awali utafanyika hapo kesho ni kuwa na maudhui mbalimbali ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

TBC inatarajiwa kuwa miongoni mwa wadau watakaochangia maudhui kutoka Tanzania kwenye chaneli hiyo mpya ya televisheni ya SABA TV.