Wambura, Sirro waapa

0
152

Rais Samia Suluhu Hassan amemvalisha cheo kipya aliyekuwa Kamishna wa Polisi Camillus Wambura ambaye amemteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Pia amemuapisha Wambura kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP).

Hafla ya kuamuapisha Wambura pamoja na viongozi wengine walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni, imefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Kabla ya kuteuliwa kuwa IGP, Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Wengine walioapishwa hii leo ni Simon Sirro aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Kamishna Msadizi wa Polisi Ramadhani Kingai yeye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambapo kabla ya uteuzi uliofanywa na Raìs alikuwa Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma.