Baridi yaua Tisa Marekani

0
902

Watu Tisa wamekufa nchini Marekani kutokana na baridi kali ambayo imelikumba eneo la nchi za Amerika ya Kaskazini, baridi ambayo inasemekana ni mbaya kutokea katika eneo hilo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Marekani na Canada zimekuwa zikishuhudia kiwango kikubwa cha theluji kikianguka, na hivyo kutatiza shughuli mbalimbali zikiwemo zile za usafiri.

Kiwango cha joto katika nchi hizo hivi sasa kimefikia nyuzi joto hasi 30 na kuna maeneo mengine kiwango hicho cha joto ni nyuzi joto hasi 40.

Safari nyingi za ndege zimefutwa katika nchi hizo za Marekani na Canada na kuwaacha wasafiri njia panda.