Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria na Uwakilishi wa nchi nyingine 14 za Afrika Magharibi, umefanya maadhimisho ya siku ya Kiswahili Duniani nchini humo.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika sambamba na maonesho ya Filamu ya Tanzania the Royal Tour, ni kutokana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), Novemba 23, 2021 wakati wa Mkutano wa 41 wa nchi Wanachama walipoipitisha Julai 7, kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili Duniani.
Uamuzi huo ulifikiwa kutokana na Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa zaidi ulimwenguni ambapo Maadhimisho hayo yaliyofanyika Jijini Abuja, yalihudhuliwa na Jumuiya ya Wanadiplomasia (kutoka Balozi za Afrika Kusini, Rwanda, Uganda, Burundi, Kenya, Congo-DRC, Bulgaria, Palestine, Burkina Faso, Cuba, Mali, Guinea, Poland na Senegal.
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Botswana nchini Nigeria, Pule Mphothwe.
Pamoja na mambo mengine, maadhimisho hayo yaliambatana na mdahalo wa wazi kuhusu ambao ulijadili kuhusu mchango wa Kiswahili katika ukombozi wa Bara la Afrika; Umuhimu wa Lugha katika ujenzi wa taifa; nafasi ya kimkakati ya Lugha ya Kiswahili katika kufikia malengo ya Eneo Huru la Biashara Barani Africa, AfCFTA changamoto na uzoefu wa kufundisha Lugha ya Kiswahili katika taasisi za elimu Afrika Magharibi.