Watu watano wamefariki dunia na wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali ya gari katika eneo la Samanda wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, imehusisha gari lenye namba za usajili T559 DGU Toyota speed suxceed lililogongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T472 DWN Toyota Wish.