Miundombinu na maeneo ya utalii kuimarishwa

0
158

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema hali ya miundombinu katika hifadhi na vivutio vya utalii inazidi kuimarishwa ili kuwezesha maeneo yote ya utalii kufikika kwa wepesi katika vipindi vyote vya mwaka, hili likifanikishwa na fedha za UVIKO19 shilingi bilioni 90.2.

Ameyasema hayo wakati akikagua banda la maliasili na utalii katika viwanja vya sabasaba yanapoendelea maonesho ya biashara kimataifa mkoani Dar es Salaam ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa 13 Agosti 2022.

Ameendelea kusema miundombinu inayoboreshwa ni pamoja na barabara ambazo zitatumika kuokoa watu wenye changamoto za kiafya ambao wameshindwa kuendelea kupanda Mlima Kilimanjaro, barabara za ndani ya hifadhi pamoja na maeneo zitakapotua helkopta kwa ajili ya kushusha kwa upesi mtalii aliyepata changamoto za kiafya akiwa juu ya mlima.

Kwa upande mwingine ameeleza kuwa wizara inaendela na mikakati yake ya kuhamasiaha utalii maeneo ya kusini mwa nchini ili kuvutia watalii zaidi katika maeneo hayo.