Usindikaji Samaki fursa sekta ya Uvuvi

0
139

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) limewataka wadau katika sekta ya uvuvi kuanzisha viwanda vya usindikaji na uchakataji wa samaki ili kuongeza thamani kwenye mazao ya Samaki.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa kilimo mifugo na uvuvi kutoka Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Peter Lushika wakati akitoa tathimini ya ushiriki wao katika maonesho ya 46 ya biashara kimataifa maarufu Sabsaba ambapo amesema wamefanikiwa kutoa elimu kwa wadau wengi wanaotembelea banda lao kuhusu fursa zilizopo kwenye sekta ya mifugo uvuvi na kilimo.

Kanali Lushika amesema wananchi waliohudhuria maonesho na kupata mafunzo ya ufugaji huo wamonesha kuwa na muitikio mkubwa kuhusu ufugaji wa samaki baada ya kufahamu eneo dogo linaweza tumika katika ufugaji hivyo kilichosalia ni kupatiwa mafunzo ya namna ya kuandaa chakula cha samaki hao.

Sambamba na hilo amesema Jeshi la Kujenga Taifa limeona ipo haja ya kuwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha chakula cha samaki ambacho ndio changamoto kubwa zaidi kwa wafugaji wa samaki kwa sasa nchini nakueleza kuwa uzalishaji huo utaongeza tija kwa sekta ya kilimo