Shauri la Mdee na wenzake laahirishwa

0
170

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha kutoa uamuzi wa maombi ya Halima Mdee na wenzake 18 ya kutaka kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hadi tarehe 8 mwezi huu.
 
Naibu Msajili wa Mahakama hiyo Elimo Massawe amesema wanaendelea kupitia hoja zilizoko mbele ya shauri hilo ili mahakama  iweze kutoa uamuzi wake kwa mujibu wa sheria.
 
Mawakili wa wabunge hao wanataka Mahakama Kuu itengue uamuzi wa CHADEMA kuwavua uanachama wateja wao kwa madai kwamba hawakupewa haki ya kusikilizwa kabla ya kuvuliwa uanachama. 
 
Novemba 27 mwaka 2020 Kamati Kuu ya CHADEMA iliwatia hatiani wabunge hao kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama.