Ufaulu form six waongezeka kwa 0.25%

0
195

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka huu na kusema ufaulu umeongezeka kwa asilimia
0.25.ikilinganishwa na mwaka 2021.

Akitangaza matokeo hayo huko Zanzibar, Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athuman Amas amesema mwaka huu ufaulu ni asilimia 99.87 ikilinganishwa na asilimia 99.62 ya mwaka 2021.

Amesema watahiniwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 wamefaulu ambapo wasichana waliofaulu ni 52, 229 sawa na asilimia 98. 55 na wavulana waliofaulu ni 52, 229 sawa na asilimia 98.55.

Amas ameongeza kuwa ubora wa ufaulu kwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja la kwanza,la pili na la tatu umeongezeka kwa asilimia 1.32 ukilinganisha na mwaka 2021

Aidha amesema kati ya shule kumi zilizofanya vizuri zaidi kitaifa, saba ni za serikali na tatu ni za watu binafsi.