Waziri Pindi Chana awaaga wanaohama Ngorongoro

0
205

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana leo Juni 30, 2022 ameshiriki zoezi la kuaga kundi la tatu la Kaya zaidi ya 25 za wananchi wanaohama kwa hiyari yao kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga.

Wananchi hao ni wale walilokuwa wakiishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambao wameamua kuhama kwa hiyari yao kuelekea Kijiji cha Msomera ili kupisha shughuli za uhifadhi.

Waziri Chana amewaaga wananchi hao akiwa na viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano nchini inayoundwa na viongozi wa Dini pamoja na uongozi wa mkoa wa Arusha akiwahakikishia kuwa Serikali chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan imewaandalia mazingira mazuri na salama katika Kijiji Cha Msomera.

Waziri Chana ameishukuru Kamati ya Amani na Maridhiano kwa uamuzi wa kwenda kujionea namna zoezi hilo la wananchi kuhama kwa hiyari linavyofanyika kwa amani na utulivu.