Wananchi wavutiwa na Gesi asilia ya TPDC

0
170

Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliounganishiwa huduma ya Gesi asilia majumbani na wanaotumia kwenye magari wameiomba Serikali Kupitia Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) kuongeza nguvu ya usambazaji baada ya kuvutiwa na Gesi hiyo.

Wananchi hao wameeleza hayo mbele ya Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Dkt James Mataragio leo alipotembelea Baadhi ya maeneo yenye nyumba zinazotumia Nishati hiyo Pamoja na kituo cha kujazia Nishati hiyo kwenye magari Ubungo.

Walter Swai Mkazi wa Sinza Dar es Salaam amesema awali kwenye shughuli zake pamoja na matumizi ya nyumbani alikuwa akitumia gunia moja la mkaa kwa la gharama ya elfu sabini kwa wiki mbili lakini kwa sasa anatumia Gesi asilia kwa gharama ya elfu 20 kwa zaidi ya siku 30.

Kwa upande wake Mkuu wa kambi za Polisi Mkoa wa Dar es Salaam Antony Mwita amewashukuru TPDC kwa kuunganisha Nishati hiyo kwenye nyumba za Polisi chang’ombe huku akieleza kuwa imeleta unafuu mkubwa kwa watumishi wa jeshi la Polisi huku Goodness Mhina akiiomba TPDC kuwasogezea watu wengi zaidi Nishati hiyo ili kusaidia utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea maeneo yanayohudumiwa na TPDC Katika kutoa Nishati ya Gesi asilia Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Dkt James Mataragio amesema mipango iliyopo ni kuwafikia Wananchi wengi zaidia ndani na nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Serikali Kupitia TPDC imeendelea Kuboresha miundombinu ikiwepo usambazaji wa Gesi asilia kwa Wananchi kwa matumizi ya kupikia, kuendeshea magari Pamoja na viwandani huku ikielezwa kuwa Nishati hiyo inasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na yenye unafuu zaidi kwa matumizi.