Muswada wa sheria ya fedha wa 2022 wapita

0
449

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2022.

Akihitimisha hoja ya serikali kuhusu muswada huo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema maoni, ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na wabunge wakati wakichangia muswada huo yamezingatiwa.

Aidha Waziri Nchemba amewataka wabunge kwenda kutoa elimu ya umuhimu wq sensa ya watu na makazi katika maeneo yao, ili serikali iweza kupanga maendeleo kulingana na idadi ya watu nchini.

Bunge #Bungeni #TBCupdates #TBConline