Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza vifo vya zaidi ya watu ishirini, vilivyotokea katika klabu moja ya usiku iliyopo kwenye mji wa East London.
Habari zaidi kutoka nchini Afrika Kusini zinaeleza kuwa, wengi wa watu hao waliofariki dunia ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 13
Mpaka sasa hakijafahamika chanzo cha vifo hivyo lakini inadaiwa kuwa vijana hao walikwenda katika klabu hiyo ya usiku ili kuungana na wenzao na kufurahia kumalizika kwa mitihani ya msimu wa baridi.
Polisi waliikuta miili ya watu hao ikiwa imetapakaa kwenye meza na viti, bila ya kuwa na dalili za wazi za majeraha.
Katika taarifa yake wizara ya Afya nchini Afrika Kusini imeeleza kuwa, kwa sasa haiwezi kutoa sababu za vifo hivyo hadi hapo itakapokamilisha kazi ya upasuaji wa miili ya watu hao na kuifanyia uchunguzi wa kina
Rais Cryil Ramaphosa wa Afrika Kusini ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu waliofariki dunia katika tukio hilo.