Wanne wafariki kwenye ajali ya treni

0
277

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 151 wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea mkoani Tabora.

Habari zinaeleza kuwa treni hiyo iliyokuwa katika safari zake ikitokea mkoani Kigoma kuelekea Dar es Salaam, imepata ajali katika eneo la Malolo.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dkt. Batilda Buriani amesema waliofariki dunia katika ajalli hiyo ni watoto wawili na watu wazima wawili.