Rais wa Chama cha Msalaba mwekundu Kimataifa(IFRC) Bwana Francisco Racco amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Uongozi wa Tanzania chama cha msalaba mwekundu Tanzania (Redcross Tanzania) na kuahidi katika miaka yake minne ijayo kuongeza msukumo zaidi kuisaidia chama hicho ili kitimize majukumu yake kwenye nyanja zote ikiwemo Afya, maafa, mazingira na maeneo mengine.
Ameyasema hayo leo tarehe 20/6/2022 mjini Geneva Uswisi, alipokutana na kufanya mazungumzo Ujumbe wa Redcross Tanzania Redcross ukiongozwa na rais wa chama hicho ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini, David Kihenzile, Katibu Mkuu Felician Mutahengerwa na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Tanzania UN , Hoyce Temu.
Francisco Racco ameasa uongozi wa Tanzania kuongeza ushirikiano na na Serikali ya Tanzania kwani ndio mdau namba moja kwenye kila Nchi.
Aidha, ameahidi kutembelea Tanzania ikiwa ni pamoja na kufika Serengeti National Park mbuga ambayo ana ndoto ya muda mrefu kuja kuiona.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania na Naibu Mwakilishi wa kudumu Nchini Uswisi, Bi Hoyce Temu akizungumza kwaniaba ya Serikali amemhakikishia Rais Racco ushirikiano wa dhati kwa maslahi mapana ya wananchi wa Tanzania.
Vikao vya Redcross Nchini Uswisi vimeanza kuanzia tarehe 18/6/2022 vinatarajia kumalizika tarehe 25/6/2022.