OSHA yasisitiza usalama mahala pa kazi

Afya na Usalama Mahala pa Kazi

0
210

Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi nchini wametakiwa kushirikiana na Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi (OSHA) ili kuhakikisha usalama na afya za watendaji sehemu za kazi unazingatiwa.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa semina iliyoshirikisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambao wamefundishwa kuhusu afya na usalama mahala pa kazi , Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana TUCTA Nice Mwansasu amesema OSHA kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kwenye matawi yao, wana wajibu wa kutembelea sehemu za kazi kukagua hali ya usalama na kupima afya za watendaji ili kuendelea kuboresha usalama na afya za wafanyakazi nchini.

Kwa upande wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha afya na usalama wa mfanyakazi unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha waajiri wanatoa huduma ya maji ya kunywa kwa watendaji kwani maji ni uhai.

Picha ya Pamoja

Semina hiyo iliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), imehudhuriwa na vijana na wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali.

Washiriki wa Semina

Katika semina hiyo limegusiwa pia suala la ukatili wa kijinsia, unyanyasaji unaotokea mahala pa kazi na ushiriki wa vijana katika kuhamasisha umoja na mshikamano ili kuwa na sauti moja yenye nguvu katika kutetea maslahi ya wafanyakazi.