Geita Gold yatakata mbele ya Dodoma Jiji FC

0
242

Geita Gold FC imepanda hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuwaadhibu maafisa wa jiji la makao makuu ya nchi, Dodoma Jiji FC kwa magoli 2 – 0.

Ushindi huo umenogeshwa zaidi na goli la George Mpole ambaye amefikisha magoli 15 akiwania kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa ligi.

Kwa kipigo hicho, Dodoma Jiji FC imesalia nafasi ya 12 ya ligi ikiwa na alama 31 baada ya kushuka dimbani mara 27.

Ligi kuu msimu wa 2021/22 imeendelea kuwa na ushindani na msisimko wa tofauti ambapo hadi sasa timu zikiingia kwenye mzunguko wa 27, bado haijajulikana timu ipi itashuka daraja, kutokana na zote kuendelea kufanya vizuri.