RC Songwe ataka majina ya wanaokwamisha miradi

0
166

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Wilaya ya Ileje ambapo ziara hii ni mwendelezo wa ziara ambayo ameianza ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi

Akiwa wilayani Ileje amemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya, Geofrey Mnauye kuwasilisha majina ya watumishi ambao ni kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Agizo hilo limefuatia baada ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwepo Shule ya Msingi Ipanga iliyopo Kata ya Mbebe, Zahanati ya Shinji iliyopewa fedha za ujenzi wa vyoo na usambazaji wa maji TZS milioni 200 ambapo baada ya ukaguzi huo Mgumba ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Badhi ya Viongozi walioambatana naye wamesema Ileje imekuwa ikifanya vibaya katika miradi ya maendeleo hali ambayo imesababisha kukosa baadhi ya fedha kutokana na uzembe katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.