Serikali yaboresha huduma kwa watu wenye ulemavu

0
1256

Serikali ya imeweka mipango madhubuti ya kuboresha huduma na mazingira katika makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam  na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira, -Anthony Mavunde kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Haji Manara Foundation  na kuongeza kuwa serikali imeweka mipango ya kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa katika masuala ya kisiasa,kijamii na ushiriki katika ustawi na ujenzi wa Taifa.

Naibu Waziri Mavunde amempongeza  Haji Manara kwa uamuzi na utayari katika kusaidia watu wenye Ualbino na kwamba serikali itatoa kila ushirikiano kwa Taasisi hiyo katika kutimiza majukumu yake hasa katika kutoa elimu kwa jamii juu ya nafasi ya watu wa kundi hilo.

Kwa upande wake Haji Manara amesema  kuwa Taasisi hiyo itasaidia kuwajengea uwezo watu wenyeUalbino pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya kuepukana na dhana potofu juu ya watu hao.

Naye mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, -Paul Makonda  ametumia uzinduzi huo Taasisi ya Haji Manara Foundation  kumpongeza Haji Manara kwa ubunifu na kuitaka jamii kuwaunga mkono watu wanaoleta mabadiliko na fikra mpya na sio kuwavunja moyo kwa maneno yasiyofaa.