KIPIGO CHASABABISHA KIFO CHA BONDIA

0
129

Bondia wa Afrika Kusini Simiso Buthelezi amefariki dunia baada ya kuvuja damu kwenye ubongo kufuatia pambano la ndondi lililofanyika Jumapili iliyopita.

 
Simiso mwenye umri wa miaka 24 alikua akipambana na Siphesihle Mntungwa kuwania taji la WBF All Africa, uzani mwepesi.

Ilipofika raundi ya 10 mpambano wa mabondia hao ulisitishwa baada ya Simiso kuonekana kuwa kivuli cha mpinzani asiyeonekana.

Picha za pambano hilo zilimuonesha Mntungwa akianguka kupitia kamba na baada ya pambano hilo kuanza tena, Simiso alisonga mbele kuelekea kwenye kona tupu ambapo alianza kupiga ngumi.
 
Mntungwa alitangazwa mshindi na baadaye Simiso alianguka na kukimbizwa hospitalini.

Aliwekwa katika hali ya kukosa fahamu baada ya kugundulika alikuwa anavuja damu kwenye ubongo.
 
Shirikisho la mchezo wa ndondi Afrika Kusini (BSA) limethibitisha taarifa za Simiso kufariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.