Idadi ya waliokufa Brazil yaongezeka

0
1232

Idadi ya watu waliokufa baada ya kuvunjika kwa kingo za bwawa moja la maji lililopo kwenye mgodi mkubwa wa chuma wa Vale nchini Brazil imeongezeka na kufikia 58.

Watu wengine zaidi ya mia tatu, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa mgodi huo uliopo kwenye jimbo la Minas Gerais  Kusini Mashariki mwa Brazil hawajulikani walipo.

Mpaka sasa vikosi vya uokoaji nchini Brazil ambavyo vimekua vikitumia helikopta 13,  vimeshindwa kuwapata watu ambao awali walidhaniwa kuwa wako hai.

Kwa mujibu wa idara ya Zimamoto nchini Brazil,  takribani watu elfu 24 wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao zilizopo katika maeneo  mbalimbali ya jimbo hilo la Minas Gerais kufuatia kuwepo kwa wasiwasi wa kutokea kwa madhara zaidi.