Barcelona tishio LA LIGA

0
1028

Timu ya FC Barcelona imeendelea kuwa tishio katika ligi soka daraja la kwanza nchini Hispania (LA LIGA),  baada ya kuitandika timu ya Girona mabao mawili kwa bila.

Mabao  ya wachezaji Nelson Semedo katika dakika ya Tisa na la Lionel Messi kwenye dakika ya 68 ndiyo yamepeleka kilio kwa Girona na kupoteza alama Tatu muhimu .

Messi sasa amefikisha mabao 26 msimu huu na kuisaidia timu yake ya FC Barcelona kufikisha alama 49 kileleni mwa msimamo wa LA LIGA.

Nao wapinzani wa wa jadi wa FC Barcelona timu ya  Real Madrid wakiwa ugenini,  wamepata ushindi mnono baada ya kuwanyuka Espanyol mabao manne kwa mawili.

Mabao ya Karim Benzema aliyefunga mabao mawili, Sergio Ramos na Gareth Bale waliofunga bao moja kila mmoja ndio yamewapa ushidi huo mnono Real Madrid na kufikisha alama 39 wakiwa katika nafasi ya Tatu kwenye msimamo wa LA LIGA.