Serengeti Girls Watua Dodoma

0
226

Timu ya Taifa ya wasichana wenye umri chini ya Miaka 17, (Serengeti Girls), asubuhi ya leo wametua jijini Dodoma tayari kuhudhuria shughuli za Bunge.

Timu hiyo iliyofuzu kwa fainali za kombe la Dunia za mwezi Oktoba chini India imealikwa Bungeni ambapo pia hii leo ndio Siku ya Bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Wakiwa nadhifu wachezaji wa timu hiyo wamesafirishwa kwa ndege aina ya Airbus A220-300 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambapo wanaotarajiwa kupokewa na kutambulishwa Bungeni asubuhi hii.