Tunahitaji viwanja vitatu zaidi kuandaa AFCON 2027

0
225

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kila mmoja akitimiza wajibu wake inawezekana Tanzania kuandaa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika 2027

Rais Samia amesema kwa sasa Tanzania inahitaji viwanja vitatu zaidi ili kufikia viwanja sita vitakavyokidhi baadhi ya vigezo vya kupewa fursa ya kuandaa michuano hiyo mikubwa barani Afrika AFCON

Katika hotuba yake Rais Samia wakati wa kulipokea kombe hilo ikulu jijini Dar es Salaam ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kesho katika uwanja wa Mkapa ili kulishuhudia kombe hilo na kupiga nalo picha ikiwa ni mara ya nne kwa kombe hilo kufanya ziara nchini Tanzania

Aidha Rais Samia amewapongeza waandaji wa zoezi hilo Coca Cola na kuwataka kushirikiana na wadau wengine ili kufanikisha Tanzania kupata uwanja mmoja wa michezo wenye hadhi ya kimataifa ili kufanikisha adhma ya Tanzania kuandaa michuano mikubwa barani Afrika

Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa Rais wa Kwanza mwanamke nchini Tanzania kulipokea kombe la dunia ikiwa ni kwa mara ya nne kwa kombe hilo kufanya ziara hapa nchini

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema wizara itaendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani michezo ni sekta muhimu inayosaidia kuendelea kuhamasisha umoja, amani na utulivu nchini

“Nchi yetu ni nchi inayopenda sana michezo ikiwemo mchezo huu wa mpira wa miguu, sisi kama wizara tutaendelea kukuunga mkono ili uendelee kuupiga mwingi” Mchengerwa