Sera na uongozi mzuri wa Rais Samia Suluhu Hassan umewezesha wanawake wengi kunufaika na sekta ya Utalii nchini kupitia kazi mbalimbali zikiwemo za kuongoza watalii, udereva, umiliki wa hoteli, ujasiriamali na vyakula vya asili
Hayo yamesemwa na Waziri Maliasili na Utalii, Dkt Pindi Chana wakati akizungumza kwenye mkutano wa wanawake wa kamati ya uongozi wa utalii Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao.
Katika mkutano huo uliojadili nafasi ya Mwanamke katika maendeleo ya Utalii, Waziri Chana amesema kuwa, ipo haja ya wadau mbalimbali hasa taasisi za kifedha kuwawezesha zaidi wanawake wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya Utalii kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu.
Amesema hatua hiyo itawainua wanawake wasio na mitaji huku akiushukuru uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kwa kuandaa mkutano huo ambao umewajengea uwezo wanawake na kujiamini katika umiliki na uendeshaji wa biashara ya Utalii Afrika.