Wananchi wa Mchinga wamshukuru Rais Samia kuzifikia kaya masikini

0
157

Wananchi mkoani Lindi jimbo la Mchinga wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoonyesha kwa vitendo kuzikomboa kaya masikini.

Wakizungumza wakati wa ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wananchi hao walioko katika kijii cha Kilangala, wanaonufaika na fedha za kusaidia kaya masikini zinazosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), walisema kupitia fedha hizo wamejiinua kiuchumi kwa kubuni miradi mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake wa Kijiji hicho, ambao wanajihusisha na mradi wa kilimo Cha mazao mbalimbali ya biashara ikiwemo minazi, Dalini Makwaya, amesema wanatoa shukrani kwa Rais Samia kwa uamuzi wake wa kutoa fedha hizo na kuwafikia moja kwa moja wahusika na hivyo kubadilisha maisha yao.

Akizungumza na wananchi hao, Shaka amesema kwa ushuhuda huo kuna kila sababu ya kuendelea kumshukuru Rais Samia ambaye amedhamiria kwa vitendo kuondoa umasikini kwa Watanzania kupitia TASAF huku akionesha matumaini makubwa kwa Mkoa wa Lindi akisema zinakwenda kuuinua zaidi kiuchumi.

“Rais Samia Suluhu Hassan anayodhamira ya dhati kabisa kuhakikisha kwamba anawatoa Watanzania katika dimbwi hili la umasikini na ndio maana amekuwa na uthubutu wa kuzungumza magumu yote badala ya kuyafunikafunika akaonyesha ama kuwapa matumaini wananchi wake ambayo tunaweza tukafika lakini tunaweza tukachelewa.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Tarek, amesema Mkoa huo ni wa kimkakati ambapo mazao yanayolimwa ni ya kibiashara akitolea mfano zao la minazi.

“Mwananchi akiwa na minazi anauhakika wa kila baada ya miezi mitatu kupata fedha. Lakini pia tuna zao la korosho ambalo ni zao linauzwa kibiashara duniani na ushahidi ukifika msimu wafanyabiashara kote duniani wanakuja mkoani Lindi kwa ajili ya kupata korosho namba moja inayopatikana mikoa ya Kusini.