Wakuu wa nchi za Afrika wakutana Malabo

0
143

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea.
 
Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili ajenda kuu mbili ambazo ni majanga, huduma za kibinadamu na masuala ya ugaidi, pamoja na mabadiliko ya Serikali yasiyozingatia misingi ya katiba.

Akifungua mkutano huo Rais wa Senegal ambaye pia ni Mwenyekiti wa mkutano huo Macky Sall amezisihi nchi za Afrika kuwa na umoja ambao utaziwezesha kukabiliana na majanga ya kibinadamu na mapambano dhidi ya ugaidi kwa urahisi zaidi.
 
Amezitaka nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano na mshikamano na kujenga uwezo wa kila nchi ili kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali ya asili.