Watoto wafariki baada ya kunywa kinywaji chenye sumu

0
203

 
Watoto watatu wa familia moja wenye umri wa miaka sita, 13 na 16 wamefariki dunia nchini Afrika Kusini baada ya kunywa kinywaji kinachodaiwa walipewa na baba yao.
 
Tukio hilo limetokea katika jimbo la Gauteng na kati ya watoto hao wawili ni wanafunzi wa shule ya msingi Ratanda na mmoja shule ya sekondari Khanya Lesedi.
 
Habari zaidi kutoka nchini Afrika kusini zinaeleza kuwa watoto hao  walifariki dunia wakiwa shuleni  na mmoja akiwa njiani kupelekwa hospitalini na inadaiwa kwamba mtoto mwingine wa familia hiyo ambaye naye alikunywa kinywaji hicho hali yake ni mbaya.
 
Familia hiyo ilikuwa ina watoto watano na ni mtoto mmoja pekee kati ya hao ndiye hajadhurika kwa kuwa hakunywa kinyaji hicho.
 
Polisi katika jimbo la Gauteng wamesema mpaka sasa haijafahamika kama kinywaji hicho kilikuwa na sumu ala la, lakini taarifa za awali zinaeleza kuwa baba wa watoto hao naye alijaribu kujiua, jambo linaloonyesha alikuwa na nia ovu.
 
Bado kuna utata kuhusu hali pamoja na mahali lipo baba wa watoto hao kwa sasa, na taarifa nyingine zinadai kuwa mama wa watoto hao naye amelazwa hospitalini.