Zanzibar inashiriki mkutano wa 75 wa Afya Duniani

0
213

Waziri wa Afya , Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akiwa katika mkutano unaojadili namna ya kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu(Global Task Force on Cholera control) unaofanyika sambamba na mkutano mkuu wa 75 wa Afya wa Dunia, Mjini Geneva, Uswisi.

Katika mkutano huo Waziri Mazrui amewasilisha uzoefu pamoja na mifano bora ya utekelezaji kwa upande wa Zanzibar katika mpango huo wa kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu (Comprehensive Cholera Eredicational Plan).

Mpango huo ni wa miaka 10 ambapo Zanzibar itashirikiana na taasisi ya GTFCC ambacho ni chombo kikuu duniani kinachoratibu mpango wa kumaliza Kipindupindu sambamba Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa (UNICEF) na taasisi ya kudhibiti magonjwa ya nchini Marekani (US CDC).