NDAKI: IDADI YA MIFUGO IMEONGEZEKA

0
196

Waziri wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema kuwa katika mwaka 2021/2022 idadi ya mifugo Tanzania imeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2020/2021.

Waziri Ndaki amesema idadi ya Ng’ombe imeongezeka kutoka milioni 33.9 hadi milioni 35

Mbuzi nao wameongezeka kutoka milioni 24.5 hadi milioni 25.6 na Kondoo wameongezeka kutoka milioni 8.5 hadi milioni 8.8.

Kuku wameongezeka kutoka milioni 87.7 hadi milioni 92.8 ambapo kuku wa asili wameongezeka kutoka milioni 40.4 hadi milioni 42.7 na kuku wa kisasa wameongezeka kutoka milioni 47.3 hadi milioni 50.1

Nguruwe nao wameongezeka kutoka milioni 3.2 hadi kufikia milioni 3.4 na hiyo ni kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mwaka 2021.

Aidha, Sekta ya Mifugo katika mwaka 2021 imekua kwa kiwango cha asilimia 5.0 sawa na mwaka 2020 na mchango wake katika Pato la Taifa umekuwa kwa asilimia 7.0 sawa na mwaka 2020.

Waziri Ndaki ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2022/2023