Mgambo waagizwa kurejesha mali za Machinga

0
226

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza Askari Mgambo kuwarudishia wafanyabiashara wadogo mali zao walizozichukua na kuziweka kwenye ‘depot’ kwa sababu mitaji yao ni midogo.

Ametoa agizo hilo akiwa ziarani mkoani Arusha ambapo amekagua masoko ya Mbauda, Kilombero na Machame na kuzungumza na baadhi ya wamachinga wanaofanya biashara kwenye masoko hayo.

Kuhusu kadhia ya Askari Mgambo, Waziri Mkuu amewataka watumie weledi na maarifa kwenye kazi yao ya ulinzi. “Mtu kama anauza eneo lililoruhusiwa, askari tumieni miongozo na waeleweshwe.”

Amewataka wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali wafanye biashara zao kwa uhuru kwa sababu Serikali inataka watimize matananio yao.

“Serikali hii inawatambua na itasimamia matamanio yenu na mtazifikia ndoto zenu. Mtaji uliowekezwa kwenye vibanda hivi na Jiji ni shilingi bilioni moja na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akaongeza shilingi milioni 500 ili masoko mengi yajengwe,” amesema Waziri Mkuu