Jackline Msongozi Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Ruvuma amepiga magoti bungeni jijini Dodoma, kushinikiza kujengwa kwa kivuko cha Mitomoni mkoani humo huku akidai kuwa kilichopo kimekuwa kikisababisha vifo.
Msongonzi amesema hayo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Amedai watu wengi wamekuwa wakifariki dunia kutokana na kuvuka katika mto Ruvuma kwa kutumia magome ya miti baada ya kukosekana kwa kivuko kinachounganisha wilaya ya Songea Vijijini na wilaya ya Nyasa.
Amesisitiza kuwa kujengwa kwa kivuko hicho pia kutachochea uchumi wa maeneo hayo kupitia mto Ruvuma.