Rais Samia Suluhu Hassan amechaguliwa na jarida maarufu duniani Times la nchini Marekani kuwa mmoja kati ya watu mia moja wenye ushawishi mkubwa duniani kwa mwaka 2022.
Wengine kwenye kundi hilo ni pamoja na Rais Joe Biden wa Marekani, Vladmir Putin wa Russia, Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine, Xi Jinping wa China , Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Aby Ahmed.
Rais Samia Suluhu Hassan aliingia madarakani mwaka 2021 kufuatia kifo cha Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli.