Maofisa Afya ya Akili na saiokolojia wanolewa

0
244

Shirika la Amref health Africa kwa kushirikiana na Shirika la PHEDES Tanzania wanaendelea kutoa mafunzo ya kutoa huduma kwa Jamii ili kuwajenga uwezo
maafisa ustawi wa Jamii, wahudumu wa Afya na azaki zianazotoa huduma za Afya ya Jamii Mkoa wa Mbeya

Mkurugenzi wa PHEDES Tanzania John Ambrose amesema wameamua kutoa mafunzo hayo Mkoa wa Mbeya kutokana na umuhimu wa kunisaidia Jamii ya watu wa Mkoa huo na kuandaa mafunzo ya siku 5 kwa wataalamu wa Sekta hiyo kutokana na matukio ya maswala ya ukatili wa kijinsia yanyokuwa yakiripotiwa kila wakati.

Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Mwanaidi Nyarukunyo amesema kesi nyingi zinazoripotiwa ni za wanawake wanaotelekezwa na wanaume waliozaa nao na wanaume hao kukimbilia Machimbo Wilaya chunya na kuacha wanawake hao wakilea peke yao familia.

Mganga mkuu wa wilaya ya Mbeya Dkt. Yahaya Msuya amesema kutokana na kuwepo kwa Barabara Kuu ya Tanzania na Zambia kunakuwa na ajali nyingi na wagonjwa wengi wakipatiwa matibabu ya majeraha wanalazimika kuwapatia msaada wa Afya ya Akili na msaada wa Kisaikolojia ili kuwarudisha katika hali ya kawaida.

Shirika la PHEDES Tanzania wakishirikana na Amref wanaendesha mafunzo ya siku tano Mkoani Mbeya kwa maafisa ustawi wa Jamii, wahudumu wa Afya na Azaki zianazotoa huduma za Afya ya Jamii kwa kuwajengea uwezo wa kutoa huduma za Afya ya Akili na saiokolojia kwa Jamii