Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika ameeleza kuwa tayari chama hicho kimefikisha barua kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu hatua ya Baraza Kuu la chama hicho kutupilia mbali rufaa ya waliokuwa wanachama 19 wa chama hicho.
Katika ukurasa wake wa twitter , Mnyika amesema barua hiyo ni ya pili baada ha ile ya Wabunge hao kufukuxwa uanachama na kamati Kuu mwaka 2020.
“Barua kuhusu Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa za waliokuwa wanachama 19 CHADEMA imeshafika kwa Spika. Hii ni barua ya pili baada ya ile ya kufukuzwa kwao uanachama na Kamati Kuu mwaka 2020. Spika ni vema akaheshimu na kutekeleza sasa matakwa ya katiba ya nchi na sheria,” ameandika Mnyika