Vituo vya Afya kupata vifaa tiba kabla ya Oktoba

0
372

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amelihakikishia bunge kuwa vifaa katika vituo vya afya mpya zilizojengwa katika maeneo mbalimbali nchini vitasambazwa kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

“Kipaumbele cha wizara ya afya ni kuhakikisha vituo ambayo vipo tayari vinaenda kuanza kazi na kuhakikisha vina vifaa na watumishi, ndani ya mwaka huu kabla ya mwezi wa kumi vituo vyote vitakuwa vimepata vifaa tiba na vitakuwa vimeanza kazi na wataalamu watakuwepo.” amesema Naibu Waziri Mollel

Dkt. Mollel ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza bungeni jijini Dodoma, swali lililoulizwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula aliyetaka kufahamu Serikali imejipanga vipi kupeleka vifaa katika hospitali mbalimbali zilizojengwa.