Waziri wa Afya Ummy Mwalimu awapongeza Wauguzi wote nchini na kuongeza kuwa anatambua juhudi zao kwani takribani asilimia 80 ya huduma zitolewazo katika vituo vya afya zinatolewa na Wauguzi.
Ametoa pongezi hizo bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ikiwa leo ni Siku ya Wauguzi Duniani.
Waziri Ummy ameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa Wauguzi, Serikali itaendelea kuajiri wauguzi wengi zaidi pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa Wauguzi wote nchini.
Aidha amewahimiza Wauguzi wote nchini kutimiza wajibu kwa kuzingatia viapo vyao ambavyo n ikuokoa maisha ya watu.