Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara kadhaa.

0
209

Rais Samia amemteua Dkt. Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu.

Dkt. Msonde amechukua nafasi ya Gerald Mweli aliyehamishiwa Wizara ya Kilimo. Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Msonde alikuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Pia amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Dkt. Kazi anachukua Nafasi ya Ramadhani Kailima aliyehamishiwa TAMISEMI. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kazi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Dkt. Switbert Mkama amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliyechukua nafasi ya Edeward Gerald ambaye atapangiwa kazi nyingine