Mauaji ya mwandishi Shireen wa Al Jazeera yalaaniwa

0
1510

Serikali ya Israel imeendelea kushutumiwa baada ya majeshi ya nchi hiyo kumuua mwandishi wa habari wa kituo cha Al Jazeera, Shireen Abu Akleh ambaye anatoka katika mamlaka ya Palestina.
 
Shireen ameuawa leo asubuhi baada ya majeshi hayo ya Israel kufanya mashambulio katika mji wa Jenin ulioko katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan katika mamlaka ya Palestina, mauaji ambayo yamelaaniwa na wapalestina.
 
Serikali ya Palestina imesema kuwa Israel imekuwa ikifanya vitendo vya ugaidi kwa kuwaua waandishi wa habari wasiokuwa na hatia, kwani tukio la sasa sio la kwanza.
 
Maandamano ya kulaani kifo cha Shireen yameendea kwenye  maeneo mbalimbali katika mamlaka ya Palestina, huku ukitolewa wito kwa Serikali ya Israel kuwajibika.