Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini -TCRA Mhandisi James Kilaba amesema mfumo mahiri ya usimamizi wa matumizi ya simu uitaleta maendeleo nchini kupitia shughuli zinazohusiana na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kuongezeka.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mhandisi Kilaba amesema mfumo huo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi na kijamii nchini.
Makabidhiano ya mfumo huo rasmi yatafanyika Januari 18 ambapo mgeni rasmi wa hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli